Tuesday, March 19, 2024

WATU 10 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUTOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHABU

Wafanyabiashara 10 wa madini wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini Mbeya.

Mavunde amesema tukio hili ni la pili kutokea Mkoani Mbeya na kuagiza kamishina wa madini kuzifuta leseni zote zinazomilikwa na watu hao pamoja na leseni zote zinazomilikea na watu hao nje ya Mkoa wa Mbeya.

Sanjari na kukamatwa watu hao na dhahabu hiyo pia vimekamatwa vifaa vya kuchomea dhahabu na mizani ya kupimia pamoja na dawa za kusafishia uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa watu wanaomiliki maeneo bila kuyafanyia kazi.

 

 

No comments:

Post a Comment