Monday, March 18, 2024

MWENYEKITI BAVICHA AJITOSA KUGOMBEA NAFASI YA UKATIBU MKOA WA SONGWE

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Songwe, Joel Silungwe amejitosa kugombea nafasi ya Katibu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) mkoani humo.

Silungwe amechukua fomu kuwania nafasi Ijumaa Machi 15, 2024 na kukabidhiwa na Paul Joseph kwa niaba ya Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Gwamaka Mbughi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fomu kwa mgombea, Mbughi amewataka wanachama kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama.

No comments:

Post a Comment