Madereva
wa Magari ya mizigo, abiria na viongozi wametakiwa kuzingatia na kufuata sheria, alama, ishara na michoro ya 
usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Kauli
 hiyo imetolewa leo Machi 25, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya 
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga wakati 
akifungua mafunzo ya muda mfupi kwa madereva wa magari ya mizigo, abiria
 na viongozi katika Chuo cha udereva cha Agility Professional Driving 
School (APDS) cha Jijini Mbeya.
Pia,
 Kamanda Kuzaga amewataka madereva wanafunzi kuheshimu watumiaji wengine
 wa barabara kwani nao wana haki ya kutumia barabara.
"Mbali
 ya vyombo vya moto kuna watumiaji wengine wa barabara, walemavu, 
watoto, wenye uoni hafifu na viziwi, hao nao wana haki ya kutumia 
barabara, waheshimuni kwa kuhakikisha mnafuata sheria, alama, ishara na 
michoro iliyopo barabarani " alisema Kuzaga.
Mkufunzi
 Mhandisi David Mtunguja kutoka chuo cha ufundi Arusha amesisitiza suala
 la umuhimu wa Dereva kulijua gari lake ili kuepuka ajali ambazo zaidi 
ya asilimia 70 zinasababishwa na uzembe wa madereva.
Mkurugenzi wa Agility Professional Driving School Mhandisi Anthony 
Malamla ameomba Serikali kuongeza nguvu ya udhibiti wa vyuo vya udereva 
ambavyo havijakidhi vigezo wala kusajiliwa ili kuepuka utapeli na 
kuzalisha madereva wasio na weledi katika taaluma ya udereva.
Jumla
 ya madereva wanafunzi 16 wa magari ya mizigo, abiria na viongozi (VIP 
Course) kutoka mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha wamefungulia rasmi 
mafunzo ya udereva ya muda mfupi katika chuo hicho kwa lengo la 
kuwajenga uwezo na weledi katika matumizi sahihi ya barabara.



No comments:
Post a Comment