Thursday, March 21, 2024

TGDC: MRADI WA NGOZI KUANZA UZALISHAJI WA JOTO ARDHI MEGAWATI 30

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) Mhandisi Methew Mwangomba amesema hatua hiyo imetokana na matokeo ya tafiti za wanasayansi kubaini uwepo wa kiwango kikubwa cha jotoardhi katika eneo hilo.

Mhandisi, Mwangomba amesema jana kwenye mkutano mkubwa wa wanasayansi kutoka mataifa mbalimbali ikiwepo Kenya. Mwangomba amesema lengo la kukutanisha wanasayansi wabobezi ni baada ya kupata matokeo mapya katika mradi wa Ngozi katika eneo la Magharibi na Kusini Mashariki .

"TGDC kwa kushirikiana na wanasayansi wabobezi kutoka mataifa mbalimbali na ukanda wa jotoardhi Afrika ikiwepo Kenya, Rwanda, Ethiopia tutajadiliana kuona namna bora itakayowezesha kuanza  uchimbaji wa rasirimali hiyo pasipo kuathiri mazingira" amesema Mwangomba.

Mwangomba amesema tafiti za kisayansi zimeonyesha uwepo wa rasirimali ya ya jotoardhi katika eneo la mradi wa Ngozi na  kubainisha kuanza kuchimba mita 1200 ili kukutana na kiwango cha  joto 250.

Amesema mikoa 16 Tanzania imebainika kuwa na  maeneo yaliyo na jotoardhi hususan kuwepo kwa  vyanzo 50 na kwamba uwepo wa rasirimali hizo utasaidia ongezeko la mapato ya taifa, ajira na uhakika wa nishati ya umeme.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara TGDC Mhandisi Shakiru Kajugus amesema kuwa mradi wa ngozi ulianza kufanyiwa tafiti mwaka 2015 na sasa umefika katika hatua nzuri ya utekelezaji.

"Kwa sasa tuko katika hatua ya uchorongaji wa visima na kufanya utafiti wa kiwango cha rasirimali ya jotoadhi kilichopo ili kuanza uendelezaji kwa ajili ya kuzalisha megawati 70 ambapo kwa awamu ya kwanza wataanza na 30 ifikapo mwaka  2025” amesema Kajugus.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mbarak Batenga amesema umefika wakati watanzania kuandaliwa kuingia kwenye matumizi ya nishati ya hiyo ili kuondokana na tatizo la umeme nchini.

"Tunaona wanasayansi kutoka mataifa mbalimbali wameshiriki mkutano huu mkubwa mbao utakuja na matokeo makubwa na mazuri ambayo yataleta chachu kwa taifa katika matumizi ya nishati mbadala ya uhakika" amesema Batenga.

Batenga amesema Tanzania itapata manufaa makubwa sana kupitia mradi huo wa jotoa ardhi kupitia miradi ya jotoardhi iliyopo wka mkoa wa Mbeya ukiwepo wa ngozi ambao unatarajia kaunza uzalishaji ifikapo 2025.

No comments:

Post a Comment