Friday, March 22, 2024

BILIONI 11 ZABORESHA HUDUMA HOSPTALI YA RUFAA MKOA WA MBEYA

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya Sh 11 bilioni kwa ajili ya kuboreshwaji miundombinu ya afya na kuchangia ongezeko la wagonjwa wanaofika kupata huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Machi 22 mwaka huu Mganga Mfawidhi Hosptali ya Rufaa Mkoa Dkt. Abdallah Mmbaga wakati akieleza mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema katika kuboreshwaji kwa huduma kati ya Sh 11 bilioni zilizotolewa na Serikali huku Sh 7 bilioni zimetumika kwa ajili ya mradi wa jengo la kisasa la upasuaji linaloweza kutoa huduma kwa wagonjwa sita kwa siku.

Amesema kuwa zaidi ya cha Sh 4 bilioni zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha ICU, nyumba za watumishi ,vifaa vya ICU, Vifaa vya EMD,Ununuzi wa Digital X-Ray na CT Scan.

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha hosptali ina wafanyakazi wenye ujuzi imetoa ajira kwa wafanyakazi wapya 34 katika kipindi cha miaka mitatu na kufanya idadi ya watumishi 410 wakiwepo wa mkataba 83.

“Sambamba na hilo uboreshwaji wa huduma  umepelekea ongezeko la wagonjwa kutoka 57,000 mpaka 132,000 ambapo awali miaka ya nyumba  wakipokea wagonjwa 4,800 mwezi hali ambayo kwa kipindi cha miaka mitatu imeongezeka na kufikia 11,000 ” amesema.

Dkt. Mmbaga amesema kuwa pia Hosptali hiyo imewezeshwa kuwa na dawa na vifaa tiba na vitenganishi vya mapambano dhidi ya uviko 19 kwa asilimia 100 ambavyo upatikana kwa muda .

Ametaja miongoni mwa bidhaa ni pamoja na chanjo ya uviko 19 dawa aina ya antibiotics sambamba na uzalishaji wa oxygen na vifaa vya vitenganishi.

No comments:

Post a Comment