Wednesday, March 20, 2024

TBL, MBEYA - UWSA, RUWASA, WAPAMBA WIKI YA MAJI KWA KUPANDA MITI 3,000

 

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA - UWSA) kwa kushirikiana na Kampuni ya bia (TBL) wamepanda miti 3,000 katika chanzo cha maji cha Mwatezi kilichopo Uyole Jiji Mbeya kwa lengo la kuhimiza utunzaji wa mazingira.

Lengo ni kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha huduma ya maji inakuwa bora na endelevu katika jamii kwa kutunza vyanzo vya maji.

Ofisa Uhusiano wa Mamlaka Neema Stanton  ameonya wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kwenye vyanzo vya Maji kwani vinachangia upotevu wa Maji kwa kiwango kikubwa.
Ametaja miongoni mwa shughuli za kijamii zinazokatazwa kwenye vyanzo ni pamoja na kama kukata miti, kilimo na ufugaji ili kutunza  miti ya asili kwa faida ya taifa na vizazi vijavyo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka, Barnabas Konga amesisitiza jamii kuwa mstari wa mbele kutunza na kuhifadhia vyanzo vya Maji kwani zimekuwa zikichangia upungufu wa Maji.

Amesema mahitaji ni lita 90 milioni huku yanayozalishwa ni lita 66.4 milioni hivyo kuna mahitaji makubwa ili kukidhi mahitaji wakati ukisubiriwa mradi wa Maji Mto Kiwira.

No comments:

Post a Comment