Thursday, April 4, 2024

TULIA TRUST YAKABIDHI KILO 400 ZA MCHELE MSIKITI MKUU WA MKOA WA MBEYA

Taasisi ya Tulia Trust imetoka kilo 400 za mchele na tende boksi 20 katika Msikiti Mkuu wa Mkoa wa  Mbeya kwa ajili ya waumini wenye mahitaji katika kuelekea sikuu ya Eid El Fitri.

Ofisa habari na mawasilino wa Taasisi ya Tulia Trust Joshua Mwakanolo amekabidhi mahitaji hayo kwa Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Msafiri Njalambaha katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya msikiti wa Mkoa barabara ya Saba jijini hapa.

Akizungumza kwa niaba ya Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson, Mwakanolo amesema lengo ni kuona wahitaji wanasherekea sikuu ya Eid El Fitri kama jamii nyingine.

"Nimesimama kwa niaba ya Mkurugenzi wa nimekabidhi mchele kilo 400 na tende boksi 20 kikubwa ni kuona wenzetu wanasherekea kwa furaha kama jamii nyingine” amesema.

Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Msafiri Njalambaha  amesema kitendo kinachofanywa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson mbali na masuala ya kisiasa amekuwa akijitolea  kusaidia watu wenye uhitaji kama  ibada kipindi cha mwezi mtukufu .

“Nimepokea futari kwa niaba ya waislamu ni kitu kinaonyesha mtu anajitoa kwa ajili ya Mungu wake watu wasimchukulue  kama anafanya kwa masuala ya kiasiasa” amesema

Naye Imani  msikiti wa Baraa Bin Azb Isanga,Shekhe Ibrahim Bombo wataendelea kumuombea Dkt. Tulia kwani amekuwa kiungo kikubwa katika kuisaidia jamii.

No comments:

Post a Comment