Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya imekabidhi magari mawili na
pikipiki mbili kwa Jeshi la Polisi ili kuongeza ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu hasa doria za barabara kuu, utoaji wa elimu na
kudhibiti ukiukwaji wa sheria za usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari Machi 04, 2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Benjamin Kuzaga katika hafla fupi ya mapokezi ya magari na Pikipiki ameishukuru Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya kwa msaada wa magari na pikipiki hizo kwani zitasaidia sana katika kufanikisha kutekeleza majukumu kwa ufanisi na haraka.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Mhandisi Rajabu Ghuliku ameeleza kuwa "Kamati
imeona vema kutoa msaada wa pikipiki na magari kwa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Mbeya ili kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu katika Kikosi
cha Usalama barabarani Mkoani Mbeya"
Aidha, Mkuu wa Kikosi cha
usalama barabarani Mkoa wa Mbeya Mrakibu wa Polisi Hussein Gawile
amesema kuwa, vitendea kazi hivyo vinakwenda kuongeza ufanisi na nguvu
katika kuzuia na kudhibiti ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.
No comments:
Post a Comment