Friday, March 1, 2024

ASILIMIA 94 WALIOTUMIA ARVs KWA USAHIHI WAMEFUBAZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI KATIKA VITUO VYA AFYA 21 VYA JESHI

Watu 23,300 Tanzania Bara na Visiwani wamefanikiwa kufikia hatua ya kufubaza maambukizi ya VVU baada ya kuzingatia matumizi usahihi Dawa za ARVs.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Shirika la HJFMRI Tanzania, Sally Chalamila amesema baada ya kukabidhi  ukarabati wa maabara mbili katika hosptali ya Jeshi Mbeya na Zahanati ya 514 KJ iliyopo Makambako Mkoa wa Njombe.

Chalamila amesema HJFMRI inatekeleza miradi miwili ikiwepo ya Nyanda za Juu Kusini na Jeshi, ambapo upande wa mradi wa Jeshi unatekelezwa katika vituo vya afya 21 Tanzania bara na Visiwani.

Chalamila amesema matumizi ya sahihi ya ARVs imeleta matokeo mazuri kwa wavvu 23,300 sawa na asilimia 94 kufubaza maambukizi na kubakiwa na moja ili kufikia 95.

“Hao watu 23,300 waliofubaza VVU, kwa  wanawake wana uwezo mkubwa wa kubeba ujauzito na kuzaa watoto wasio na maambukizi, hata kuambukiza wenza wao na wataendelea kuishi salama kabisa kama jamii nyingine” amesema.

Amesema HJFMRI itaendelea kuboresha huduma za maabara ili kusaidia upatikanaji wa vipimo vya wavvu na kuanzishiwa Dawa mapema na watumie kwa usahihi ili kufikia mpango wa malengo ya serikali ya 95-95-95.

Kwa upande wake Meneja mradi wa Jeshi kutoka Shirika la HJFMRI, Dk, Anastazia Masanja amesema kuwa faida ya ukarabati wa miundombinu ya majengo ni kuongeza uwezo wa kiuchunguzi na kushughulikia idadi kubwa ya vipimo.

Amesema  itasaidia kupunguza muda wa wateja na kuruhusu ufuatiliaji wa kina zaidi wa maendeleo ya matibabu ya VVU kwa wagonjwa sambamba na uboreshwaji wa maabara ambao utasaidia wafanyakazi kufanya kazi kwenye mazingira bora na salama.

“Kuboresha majengo ya maabara kuna kidhi viwango vya udhibiti wa mahitaji ya kupima na ufuatiliaji pamoja na kuzingatia itifaki za usalama, uthibiti ubora kulingana na viwango vya wizara ya afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma za tiba Jeshini Brig. Gen. Charles Mwanziva amesema Jeshi lina vituo 21 nchini ambapo asilimia 70 ya wanaofika kupata matibabu ni raia kutoka maeneo mbali mbali.

“Kimsingi tunaashukuru Shirika la HJFMRI, kwa kuboresha na kupanua miundombinu ya vyumba vya maabara itaongeza ufanisi wa utoaji huduma na hata wataalam kuwa salama kwani awali kulikuwa na ufinyu wa vyumba” amesema.

Ameongeza kuwa pia huduma zimeboreshwa hususan uwepo mashine za kisasa za CT Scan na MRI ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fedha sambamba na uwepo wa madaktari wazuri wanaotoa huduma kwa wagonjwa wa ndani na nje.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Utafiti ya Walter Reed Army Institute of Research (WRAIR) ya Idara ya Ulizi ya Marekani Mark Breda amesema wataendelea kushirikiana na Serikali kupitia vituo vya Jeshi kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa hususan mapambano ya VVU.

No comments:

Post a Comment