Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoa wa Mbeya (TPF Net) ukiongozwa na Mwenyekiti wake Mrakibu wa Polisi (SP) Kaneng Muro umepamba kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia ambayo kimkoa yamefanyika Ubaruku, Wilaya ya Mbarali.
Pia,
mtandao wa Polisi wanawake mkoani hapa kwa kushirikiana na Dawati la
Jinsia na Watoto umekuwa kivutio kwa washiriki wa maadhimisho hayo
ambapo elimu kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi
ya watoto na wanawake ilitolewa.
Sambamba na hilo, kikosi cha usalama barabarani kilipata nafasi ya kueleza matumizi ya kidigitali ya ukusanyaji wa madeni ya makosa ya usalama barabarani, vipimo vya ulevi kwa madereva na ukamataji wa makosa ya ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani kwa kutumia "POS Machine".
Mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mwanamke dunia kwa Mkoa wa Mbeya alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera huku maadhimisho yamebeba kauli mbiu "Wekeza kwa Wanawake, Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".
No comments:
Post a Comment