Ikiwa
ni kiliele cha Madhimisho ya Siku ya Wanamke Duniani ambayo
huadhimishwa machi 8 kila mwaka, Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa ya
Kanda Mbeya leo Machi 08, 2024 wamekabidhi hundi yenye thamani ya
shilingi Mil 37.5 kwaajili ya ununuzi wa kitanda cha kisasa kwaajili ya
Upasuaji wa mifupa hospitalini hapo.
Akipokea hundi hiyo ya Mil
37.5 Dkt. Godlove Mbwanji ,Mkurugenzi Mtendaji wa Hospotali ya Rufaa ya
Kanda Mbeya ameushukuru na kuupongeza Umoja wa Wanawake Hospitali ya Rufaa
ya Kanda Mbeya kwa kuwa chachu na mchango mkubwa katika maendeleo ya
Hospitali na mkoa kwa ujumla.
“...ninyi mmekuwa ni chachu kubwa
sana kwa mafanikio ya hospitali na mkoa kwa ujumla nichukue nafasi hii
pia kuwapongeza wanawake wote Tanzania nzima kwa mchango mkubwa sana wa
maenedeleo ya nchi yetu.” Dkt. Godlove mbwanji
Sambamba na hilo
Dkt. Mbwaji ametoa rai kwa akina baba kuweka jitahada zaidi katika
malezi ya mtoto wa kiume ili kujenga taifa lenye vijana imara katika
jamii.
“...lakini sasa hebu tuwatazame watoto wa kiume na hii
sio kwa akina mama ni kwa upande wa akina baba pia ili mwisho wa siku
tuwe na taifa lenye vijana imara.” Dkt. Godlove Mbwanji.
Akiongea
wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Joyce Komba, katibu wa umoja huo
amesema lengo la kukabidhi zawadi hiyo ni kurudisha fadhila kwa jamii
pamoja na kuushukuru Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa
kuwaongoza katika misingi imara inayopelekea kutoa huduma bora kwa
wagonjwa na kudumisha umoja, upendo na mshikamo.
“..zawadi hii ni
sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na kushukuru uongozi wa
hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kutujenga katika misingi imara
pamoja na kudumisha umoja na mshikamano kwa watumishi” Joyce Komba
Dkt.
John Mbanga ni mkuu wa idara ya upasuaji hospitali ya Rufaa ya Kanda
Mbeya, ameshukuru kwa zawadi hiyo na kusema upatikanaji wa kitanda hicho
umekuwa msaada mkubwa sana hasa katika kipindi ambacho ajali zimekuwa
nyingi na kusema kitanda hicho ni cha kipekee na kisasa kitakachopelekea
huduma ya upasuaji wa mifupa kufanyika kwa urahisi zaidi.
No comments:
Post a Comment