Mbalaza wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa
 kutoka Mkoa wa Mbeya Timida Fyandomo ametembelea eneo la ujenzi wa 
nyumba ya muhitaji anayejengewa na taasisi ya Tulia Trust katika kata ya
 Iganjo Mbeya Mjini.
Akiwa katika eneo hilo Timida ameahidi kutoa
 Godoro kumsaidia muhitaji huyo ikiwa ni kuunga mkono jitihada 
zinazofanywa na Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi wake ambaye 
ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge na  Mbunge wa 
Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson.
Nyumba hiyo inayojengwa kupitia mpango wa Tulia Trust Mtaani Kwatu 
inatarajiwa kukabidhiwa kwa mlengwa huyo mapema mweezi Aprili mwaka huu.
Kwa
 upande wake, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, 
Joshua Mwakanolo amesema ujenzi wa nyumba hiyo iko katika hatua za 
mwishoni.
Amesema wanatarajia mara baada ya kukamilisha ujenzi 
huo uzinduzi utafanywa na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika 
wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson ambaye pia ni 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust.


No comments:
Post a Comment