Tuesday, March 12, 2024

WANAFUNZI 3,000 WAPEWA MADAFTARI BURE JIJINI MBEYA

Taasisi ya Tulia Trust ambayo Mkurugenzi wake ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge  Dkt. Tulia Ackson imetoa madaftari 600,000 kwa wanafunzi 3,000 wanaoishi katika   mazingira magumu.

Msaada huo utagusa shule 70 katika Kata 36 za Jiji la Mbeya sambamba na kutoka viti mwendo kwa watu wenye ulamavu zaidi ya 36 ikiwa ni maelekezo ya Mkurugenzi wa Taasisi hiyo kuwagusa wahitaji.

Ofisa elimu msingi Kata ya Uyole akizungumza mara baada ya kupokea madaftari.

“Kupitia maelekezo ya Mkurugenzi wa Taasisi Dkt. Tulia ni kugusa walengwa shule za msingi 70  ambapo zaidi ya madaftari 600,000 yaliyotolewa kwa wanafunzi 3,000 huku idadi yake italingana na darasa analosoma mlengwa” amesema.

Amesema huo ni mpango endelevu wa kuchangia sekta ya elimu kwa lengo la kutimiza ndoto za vijana kupata elimu bora na kuwa chachu kwa taifa.

Hata hivyo amesema wananchi wanapaswa kumuombea Dkt. Tulia ili atimize yale ambayo amepanga kusaidia wahitaji na kwamba sio kwamba anautajiri bali ni kipawa alichopewa na Mwenyezi Mungu.

Ofisa elimu msingi Kata ya Uyole, Lucas Komba amesema tangu Dkt. Tulia amekuwa na mchango mkubwa kwa Serikali, jamii na siasa na kwamba msaada huo itakuwa chachu ya kuongeza ufauru.

“Siku za nyuma tulikuwa na changamoto ya utoro kutokana na kukosa mahitaji lakini baada ya kupata sare za shule mahudhuria yamekuwa mazuri sana na matarajio ni Shule za serikali kufanya vizuri” amesema.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Hasanga Alphonce Mkuchika, amesema kuna wanafunzi 1,150  huku 37 wamenufaika na mgao wa sare za shule wa madaftari halo ambayo imeongesa hali ya kupenda masomo.

No comments:

Post a Comment