Monday, March 11, 2024

MASACHE AFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO JIMBONI


Mabunge wa Jimbo la Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Masache Kasaka amefanya ziara ya  kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwepo miradi ya sekta ya Elimu ambayo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan  ilitoa fedha.

Katika ziara yake Masache ametembelea Kata ya Itewe sambamba na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Chunya mjini.

Masache amesema kuwa katika mradi wa shule ya msingi Chunya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi  ya Sh 90 milioni.

“Nina kila sababu ya kuishukuru Serikali ya awamu ya sita kwani imetuletea fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika miundombinu ya barabara,maji na miundombinu ya elimu”  amesema.

Pia Masache alichangia mifuko 40 ya saruji kwaajili ya ujenzi wa madarasa 4 vilivyojengwa kwa nguvu za wananchi.

No comments:

Post a Comment