Thursday, March 28, 2024

DIWANI MATUNDASI AWAPA TABASAMU KWA WALIMU MSINGI NA SEKONDARI CHUNYA


Diwani Kata ya Matundasi Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Kimo Choga ameandika historia kwa  walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kwa kutoa motisha baada ya kuridhishwa na kupanda kwa ufauru  wa wanafunzi .

Choga amefanya tukio hilo jana katika hafla fupi aliyoandaa kwa kuwatanisha walimu, watumishi wa serikali viongozi na Chama cha Mapinduzi (CCM) sambamba na Madiwani kutoka baadhi ya Kata Wilaya ya Chunya.


Akizungumza walimu na watumishi wa serikali amesema kuwa amewiwa kutokaa ndani ya Moyo wake kufanya tukio hilo kwa kutambua mchango wa walimu katika kuchochea sekta ya elimu hususani kwa Shule ya Sekondari Makalla.

“Hili ni wazo nilikuwa nalo na nilishirikisha viongozi, wakuu wa shule, maofisa elimu kuwepo na mpango wa  kufanya tukio hilo kuona tunakaa kula pamoja na kubadilishana mawazo na walimu, kama Diwani matokeo mazuri ya sekta ya elimu yananipa sifa kubwa” amesema.

Ameongeza kuwa “Nitahadhalishe kwa hiki ninachokifanya  hapa isije kuhusishwa na masuala ya kisiasa kwani tunaelekea kwenye uchaguzi lisije kubebwa kwa tafsiri hiyo” amesema.

Choga amesema ili kuboresha sekta ya elimu kufanya vizuri zaidi ni vyema walimu kuwakumbuka kwa  kutoa motisha kwa wale ambao wamekuwa na mbinu mbalimbali za ufundaji na kusaidia wanafunzi kufanya vizuri lengo la kuwapa hamasa ya kuongeza weredi na mbinu ya kufanya vizuri zaidi” amesema.

Wakati huo huo amesema ataendelea kushirikiana na kutatua changamoto za walimu pale inapobidi sambamba na kuomba Serikali kutenga fedha miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu na barabara ili kusaidia kuchochea shughuli za kiuchumi.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hassan, na uongozi wa Halmashauri kwa kutoa fedha kuchochea sekta ya elimu hususani ujenzi wa vyumba 8 vya madarasa Shule ya Sekondari  Makalla na hatua ya kuanza ujenzi wa mabweni mawili ya wanafunzi kike ili kuwaondoa na adha ya kutembea umbali mrefu".

Mjumbe Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Mbeya na Diwani viti maalum kata ya Chalangwa, Phidekatwila Mwalukasa amempongeza Diwani Kata ya Matundasi kwa kuona umuhimu wa kuwakumbuka walimu na kutoa motisha kama kuongeza hamasa katika ufundishaji.

“Hili ni jambo kubwa sana ulilofanya mwanangu Choga, tunatambua walimu wanapitia changamoto kubwa lakini wameweza kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya elimu ya msingi na Sekondari na kutupa tabasamu” amesema.

Pia amewataka walimu na watumishi kuwa Serikali inawathamini na kutambua mchango wao na tegemezi  katika kuelekea uchaguzi mdogo wa Serikali za mitaa na Mkuu 2025.

Diwani viti maalum Makongorosi, Sophia Mwanautwa amesema wataendelea kutoa ushirikiano kwa Diwani wa Kata ya Matundasi kwani amekuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha sekta ya elimu inafanya vizuri kwa kutoa motisha kwa walimu.

Kaimu Ofisa Elimu Msingi Wilaya ya Chunya, Jeras Shutindi amewataka walimu kuongeza jitihada za kufanya vizuri zaidi kuhakikisha wanakuwa chachu ya kuongeza ufauru kwa wanafunzi wa elimu ya msingi na Sekondari sambamba na kujiendeleza.

“Msiridhike na viwango vya elimu mlivyo navyo jiendelezeni ili kuweze kupanda madaraja na kuwa chachu zaidi katika sekta ya elimu nchini na sio Chunya Pekee".

No comments:

Post a Comment