Tuesday, October 29, 2024

WASHINDI TULIA STREET TALENT COMPETITION 2024 KUPELEKWA BAGAMOYO

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amesema walioibuka washindi mashindano ya Tulia Street Talent Competition kuendelezwa kituo cha sanaa na utamaduni Bagamoyo.

Dkt. Tulia amesema Oktoba 27 mwaka huu wakati wa kuhitimisha mashindano hayo huku mgeni rasmi  msanii mkongwe Naseeb Abdul (Diamond Platnam) ambayo yalifanyika kwa siku tatu mfurulizo ikiwa ni msimu wa tano.

"Sisi kama Tulia Trust tunawa andaa na kuibua vipaji ili watakao wahitaji watawatafuta lakini pia niombe Daimond useme neno ili vijana hawa wapone" amesema.

Dkt. Tulia amewataka washindi wa Tulia Street Talent Competition 2024 kuwa chachu na zawadi wanazopata zikawatoe sehemu moja kwenda nyingine" amesema .

Amesema wasanii walioibuka washindi watapata fursa ya kwenda kujifunza zaidi katika Taasisi ya  Sanaa na Utamaduni Bagamoto.

"Hizo zawadi mnazopata tumieni kama fursa kutoka sehemu moja kwenda nyingine na sio kuelekeza kwenye matumizi mengine na kusisitiza Taasisi ya Tulia Trust wataendelea kuandaa matamasha mbalimbali" amesema.

Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul "Diamond Platnam amesema kupitia kampuni yake ya Wasafi Media ataungana na Taasisi ya Tulia Trust kuandaa matamasha na kuonyesha live.

Amesema atafungua studio ya kisasa kwa ajili ya kurekodi kazi za wasanii wanaoibuliwa kupitia matamasha yanayoandaliwa na Taasisi ya Tulia Trust.

"Nikupongeze sana Dkt. Tulia kwa kuandaa matamasha ya kuibua vipaji kwa vijana nikuhakikishie ntashirikiana na Tulia Trust kwa kuonyesha live kupitia wasafi media ili watanzania waweze kutazama na vijana wapate ajira" amesema.

No comments:

Post a Comment