Tuesday, October 8, 2024

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI WAAPISHWA WAONYWA MATUMIZI YA POMBE

 Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Oktoba 8, 2024 imefanya zoezi la kuwaapisha wasimamizi wa uchaguzi zaidi ya 200 ngazi za mitaa katika kuelekea zoezi la uandikishaji wananchi kwenye daftari la kudumu la wapigaku.

Zoezi hilo limefanyika katika Ukumbi wa Mkapa Jijini hapa kwa  kula kiapo mbele ya Hakimu wa Mahakama wa Wilaya Mkoa wa Mbeya .

Awali akizungumza baada ya kuapishwa, Msimamizi msaidizi wa uchaguzi Jiji la Mbeya Oddo Nduguru amewaonya wasimamizi kuepuka matumizi ya vilevi wakati wa kuendesha zoezi hilo ili kutunza siri za kiapo walichopewa.

"Tunaelekea zoezi la Uandikishaji Daftari la kudumu la wapigakura litakaloanza Oktoba 11 mpaka 20 mwaka huu kwa wale wanatumia vilevi tunaomba wakawe wavumilivu kwa siku 10 za kuendesha zoezi hilo" amesema.

Oddo amesema kitendo hicho kinaweza kuzua taharuki kwa jamii na kusisitiza kuzingatia miiko ya kanuni za uchaguzi na muda ulipangwa kuwasili kwenye vituo.

Ofisa uchaguzi Jiji la Mbeya Gregory Emmanuel ametoa maelekezo ya ushiriki katika zoezi la  uandikishaji sambamba na kuzingatia elimu ya semina  elekezi waliyopewa .

Naye Ofisa mtendaji kata ya Sisimba na Msimamizi msaidizi wa uchaguzi, ametoa maelekezo ya maswali yasiyostahili kuhojiwa wapigakura kama, udini, ukabila, ufuasi wa vyama na ajira.

Aidha amefafanua kuwa majengo yasiyo stahili kuandikisha wapigakura misikiti, makanisa, magereza na miundombinu ya ofisi za  vyama vya siasa.

Aidha ametoa maelekezo ya wasimamizi wa uchaguzi kutowatilia mashaka mawakala wa vyama vingine vya upinzani kwani wana haki ya kushiriki kuona mwenendo wa zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment