Thursday, October 10, 2024

AGRICON BORESHA CHAI YANUFAISHA WAKULIMA MBEYA, NJOMBE, IRINGA

 

Wakulima zaidi ya  22,000 Mikoa ya Mbeya,Njombe na Iringa wamenufaika na  mafunzo ya shamba darasa kupitia mradi  Agricon Boresha  Chai uliotekelezwa na Shirika la IDH Tanzania kwa ufadhiri wa Jumuiya ya Ulaya (EU)

Meneja mradi wa Shirika hilo  ,Elikinda Tenga amesema  jana Oktoba 9,2924  wakati  wa  Mahafari ya  Mafunzo ya  Wakulima ya Shamba  Darasa(FFS)  yaliyofanyika katika kijiji cha Syukula Kata ya Kyimo Wilaya ya Rungwe

Amesema  mradi wa Agricon Boresha chai umelenga kuwajengea uwezo wakulima na kuwezesha upatikanaji wa  vifaa vya kisasa na matumizi ya teknolojia kutumia matone kunyunyiza kwenye mashamba.

Ameongeza  mradi huo umetekelezwa kwa kipindi cha miaka minne huku zaidi ya Sh 537.2 milioni zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa na magari ya kusafirisha chai kuingiza sokoni huku wilaya ya rungwe ikinufaika na Sh 224.7 milioni."amesema.

Ofisa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Wilaya ya Rungwe,Stephen Mbiza amesema kupitia mradi huu wakulima wamenufaika na miche 389,000 kati ya miche 600,000 iliyozalishwa kupitia mashamba darasa waliyopewa.

Amesema kamaserikali wataendelea kushirikiana na wadau katika kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya kilimo kwa wakulima wa   chai wilayani humo.

Mratibu wa Chama cha Kilimo na Masoko cha wakulima wadogo wa chai wilaya ya Rungwe na Busokelo,(RBTC -JE) Richard Mlelwa ameomba serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza bei kutoka Sh 360 kwa kilo ambayo wameuza kwa miaka mingi  sasa.

"Kwa sasa bado kuna wakulima wanazalisha kwa mazoea lakini tunashukuru ujio wa mradi huo umeweza kuwabalisha na kugeukia kilimo tija licha ya changamoto ya soko na pembejeo za kilimo"amesema.

 Baadhi ya wakulima wamelalamikia ukosefu wa masoko ya chai na uhakika wa pembejeo za kilimo hali inayodumaza uzalishaji wa tija na kuomba  serikali kuwawezesha

No comments:

Post a Comment