Chuo Kikuu Katoriki Mbeya (CUoM) kimefanya kongamano la kumbukizi la miaka 25 ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kama sehemu ya kuenzi mchango wake katika kulitumikia taifa.
Kongamano hilo limefanyika Oktoba 25 mwaka huu huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere lililoshirilisha wadau wakiwepo wanafunzi maprofesa na madaktari kutoka vyuo mbalimbali.
Akizungumza kwenye kongamano hilo Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Rumuald Haule amesema uongozi wa chuo unatambua mchango mkubwa wa hayati Mwalimu Nyerere katika kusimamia sekta ya elimu ya ujamaa na kujitegemea.
"Kumbukizi hilo lina tija kwa wanafunzi kujua historia ya Taifa la Tanzania lililotoka mpaka nchi kupata Uhuru kwa kujenga umoja, upendo amani na mshimano" amesema.
Haule amesema kama chuo wataendelea kufanya kumbukizi kama chachu ya kutumia uwekezaji katika sekta ya elimu na kuwepo kwa mitaala ya elimu ya kujitegemea ili kuwaandaa vijana kuwa wazalengo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amesema kuwa mwalimu alikuwa ni mtu wa kipekee aliyelipigania taifa kabla na baada ya kupata uhuru.
"Watanzania tusiichezee hii amani iliyoachwa na Baba wa Taifa ambaye aliona mbali zaidi kuanzia Taasisi mbalimbali kwa lengo la kujenga umoja mshikamano na kuhakikisha lisiteteleke" amesema Makongoro.
Wakati huo maprofesa na wanafunzi wa CUoM wameomba mitaala ya lugha ya kiswahili ipewe kipaumbele vyuoni ili kuenza utamaduni wa mtanzania badala ya lugha za kigeni.

No comments:
Post a Comment