Thursday, October 24, 2024

DKT. TULIA AGAWA MITUNGI YA GESI KWA MAMANTILIE WA SOKO LA MATOLA

Mbunge wa Mbeya mjini na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson amegawa mitungi ya nishati gesi bure kwa mamantilie 25 katika soko la  Matola jijini hapa.

Hatua ya Dkt. ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Dunia (IPU) kugawa mitungi na nishati safi ya gesi ni kuhamasisha mama lishe kuachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo sio salama kwa afya.

Akizungumza mara baada ya zoezi la kugawa mitungi kwa Mama ntilie 25 amesema hiyo ni sehemu ya ahadi yake lakini pia ni kuunga mkono juhudi za Mh Rais Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo.


"Lengo si kwa matumizi tu bali ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya gesi lakini pia nimetoa mabati 16 kwa ajili ya kufanya maboresho ya paa ili mfanye kazi katika mazingira rafiki na  salama"amesema Dkt. Tulia .

Pia Mbunge huyo Dkt. Tulia amewatembelea vijana wanaojihusisha na shughuli za uoshaji wa magari katika eneo la mafiati jijini hapa lengo ni kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mh. Dkt. Tulia Ackson, leo Oktoba 24, 2024 ametimiza ahadi yake kwa kukabidhi mitungi ya gesi 25 kwa mama ntilie wa soko matola aliyoitoa jana ili kuepukana na matumizi ya mkaa na kutumia nishati safi.

Wakati huohuo Dkt. Tulia amewapatia mabati 16 ili kukarabati paa la soko hilo ili kujikinga na jua na  mvua.


No comments:

Post a Comment