Wednesday, October 23, 2024

WANANCHI 188,644 WAJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA WILAYANI CHUNYA

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya Mubarak Batenga amesema asilimia 89 ya watu 188, 644 wameji andikisha kwenye daftari la wapiga kura na kutarajiwa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa  Novemba 27 mwaka huu.

Batenga amesema jana Oktoba 22, 2024 wakati akifungua Kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya mwaka 2024/25 cha kujadili taarifa ya fedha na makusanyo ya mapato ya ndani huku wakiwa wamevuka malengo na kufikia Sh 12.5 bilioni.

Amesema kufuatia taarifa ya daftari la wapiga kula madiwani warejee kutoa elimu ya uhamasishaji ili wote waweze kupiga kura kuchagua wenyeviti na wajumbe wa serikali za mitaa ifikapo Novemba 27 Mwaka huu.

"Madiwani kama mlivyohamasisha katika mchakato wa awali rejeeni tena kwa wananchi kutoa elimu ya umuhimu wa kupiga kura ili tupate asilimia 89 tarajiwa na sio vinginevyo" amesema.

Batenga amesema matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu yataonyesha taswira ya nafasi zenu kupenya katika uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 wa kuwania nafasi za Ubunge, Udiwani na Rais.

"Imebaki miezi michache kufikia uchaguzi Mkuu Oktoba 2025 niwasihi madiwani hamasisheni wananchi kujitokeza kupiga kura kama mlivyofanikisha katika uandikishaji daftari la wapiga kura na kuandaa viongozi wazuri wa serikali za mitaa" amesema.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya na Diwani wa Mamba Ramadhan Shumbi amewataka madiwani kutumia kipindi hiki cha uchaguzi kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye  uchaguzi wa serikali za kupiga kura kwa kuchagua viongozi kutoka CCM.

Katika hatua nyingine amepongeza madiwani kwa ushirikiano wao kusimamia ukunyaji wa mapato na kuwezesha kuvuka malengo kwa kufikia wastani wa Sh 12.5 bilioni na kutoka asilimia 40 mpaka 60 ya makusanyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Afisa Utumishi na Utawala John Felix amehamasisha watumishi kuchapa kazi kwa weredi kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa umma na si kujihusisha na utoro na ulevi kazini.

Amesema nidhamu ya kazi ni njia pekee ya kuwajibika hivyo ni vyema kutekelezaa majukumu yao kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma katika ngazi ya serikali.

No comments:

Post a Comment