Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya limemwazimia kumfukuza kazi Ofisa mtendaji wa kijiji cha Matwiga Samweli Koko kwa madai ya kukithiri kwa vitendo vya ulevi, utoro na matumizi mabaya ya madaraka.
Hatua hiyo imefikiwa jana Oktoba 22, mwaka huu baada ya kikao cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kukutana kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2024/25 sambamba na kufanya maamuzi kuhusiana na tuhuma hizo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chunya, Ramadhan Shumbi amesema wamefikia hatua hiyo kufuatia kukithiri kwa tabia hizo licha ya kumkanya mara kadhaa.
Amesema kutokana na mwenendo wa tabia zake wamejaribu kumuita na kumkanya lakini ameshindwa kubadilika hali iliyopelekea baraza la madiwani kufikia uamuzi ya kumwazimia kumfukuza kazi.
"Katika utendaji wake wa kazini ana zaidi ya mwezi hajaripoti kituo chake cha kazi ambapo ni kinyume cha taratibu za utumishi wa umma pasipo kutoa taarifa kwa mwajiri wake" amesema.
Shumbi amesema hali hiyo imekuwa ikikwamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kibaya zaidi wakaguzi wakifika eneo lake la kazi kukosa ushirikiano.
Kwa upande wake, Afisa utumishi na utawala John Felix amesema kabla ya kumfukuza kazi walimuita na kumkanya ambapo aliomba radhi lakini amekuwa akirudia utoro kazini na ulevi wa kupindukia.
"Licha ya kumuandikia barua za onyo tuliunda tume ya kumchunguza mara mbili ambayo ilimbaini kuhusika na ulevi, utoro kazini na wizi wa fedha za umma" amesema Felix.
Amesema hatua za kumuondoa kazini wamezingatia tararibu zote za kisheria sambamba na kuonya watumishi wengine kuepuka matumizi mabaya yaa madaraka ikiwepo utoro kazini ulevi na ubadhirifu wa mali za umma.
Kwa upande wake mtendaji huyo alipohojiwa na Mwandishi wa habari hakuweza kutoa ushirikiano kwa kueleza atapiga simu kwa madai yuko sehemu mbaya.

No comments:
Post a Comment