Halmashauri ya Jiji la Mbeya limewaapisha mawakala wa vyama vya siasa leo Oktoba 10, 2024 katika ukumbi wa Mkapa Jijini hapa.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya Teddy Mlimba amewaapisha mawakala hao huku viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakishiriki na kutoa maoni yao kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.
Ofisa uchaguzi Jiji la Mbeya Gregory Emmanuel amesema uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu utakuwa wa huru na kuzingatia demokrasia ya mifumo ya vyama vingi.
"Mawakala mkazingatie mwongozo wa kanuni na sheria katika zoezi la uandikishaji wapiga kura linalotarajiwa kuanza kesho Oktoba 11 mpaka 20 mwaka huu katika vituo zaidi ya 211 jijini hapa" amesema.
Emmauel amewataka viongozi wa vyama vya upinzani kutekeleza sheria na matakwa ya uchaguzi kuzingatia mwongozo wa uchaguzi unavyosema.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Hamadi Mbeyale ameomba utaratibu wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu usiwe na vikwazo kama yaliyotokea mwaka 2019.
Mmoja mawakala wa Chadema Furaha Mwaijumba amesema ili elimu iweze kuwafikia wananchi walio wengi kutokana na jiografia ya Jiji la Mbeya wapewe nafasi kutumia gharama zao kufikisha matangazo maeneo mbalimbali ili kuwezesha kuhamasika na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.

No comments:
Post a Comment