Friday, October 4, 2024

NCHIMBI AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUHAMASISHA WAUMINI KUPIGA KURA

Msimamizi wa Uchaguzi Mdogo wa Serikali za mitaa Jiji la Mbeya John Nchimbi amewaomba viongozi wa dini,machifu kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kushiriki  katika uchaguzi Novemba 27, 2024 kuchagua viongozi bora.

Nchimbi amesema leo Ijumaa Oktoba 4, 2024 kwenye kikao kilichohusisha viongozi wa dini,machifu wadau na viongozi wa vyama siasa kilicholenga kutoa maelekezo kuelekea uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa.

Nchimbi amesema kuwa mchakato wa kuelekea uchaguzi umekamilika hivyo wananchi wajitokeze kushiriki kikamilifu hususani kujiandisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura ikiwa ni wajibu wao wa kikatiba.
"Kuchagua kiongozi anayefaa ni wajibu wakila mtanzania kutimiza na kutekeleza ili kuleta maendeleo  ili kulifikisha jiji letu sehemu sahihi" amesema Nchimbi.

Amesema ni jukumu la viongozi wa dini kulipa uzito wa kipekee suala la uchaguzi lengo ni kuona kila mtanzania anachagua kiongozi wa serikali za mitaa ambaye ataleta tija na si kuleta malumbano.

"Jamani wagombea watapita huko kuomba kura msiwachukie waonyesheni upendo mkisubiri siku muhimu ya kupiga kura 27 Novemba" amesema na kusisitiza uvumilifu.

 Meya wake Jiji la Mbeya amehamasisha viongozi wa dini,mira kuhubiri suala la uchaguzi kwa kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu na  kupiga kura lipewe kipaumbele.

"Sisi wote ni watanzania niwaombe sana katika uchaguzi ujao uwe wa haki, amani na uhuru wa kidemokrasia kwa kuchagua viongozi sahihi na kuleta machafuko" amesema.

Issa amesema uchaguzi ni uchaguzi tu watakaopewa fursa ya uongozi na watakao kosa kuwa wavumilivu na kudumisha amani ya kweli kwa kuungana ili kuleta maendeleo ya kweli.

Wakati huo huo amewataka watanzania wenye sifa ya kugombea nafasi mbalimbali wajitokeze   kuchukua fomu ya kugombea na sio kupoteza haki yao ya msingi ya kikatiba.

No comments:

Post a Comment