Tuesday, October 15, 2024

MBUNGE WA LUPA ALIA NA TRA UTITIRI WA KODI WACHIMBAJI WADOGO

Mbunge wa Lupa Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya, Masache Kasaka ameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kupunguza utitiri wa tozo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu.

Masache amesema Oktoka 14 ikiwa ni usiku wa madini ambayo Mkoa wa Mkuu wa Mkoa Juma Homera alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri wa Madini Athon Mavunde.

"Tukuombe Mkuu wa Mkoa tuwasilishie kilio chetu kwa Waziri mwenye dhamana kutazama changamoto ya cha utitiri wa tozo kwa wachimbaji wadogo ili kuwezesha kuendesha shughuli zao na kutokwepa kulipa kodi" ameseme Masache.

Amesema Wilaya ya Chunya kitaifa tunashika nafasi ya pili sambamba na mchango mkubwa kwa pato la taifa kutokana na mauzo ya dhahabu kuwa juu.

Masache amesema endapo serikali ikiondoa changamoto hizo uenda shughuli za uchimbaji zikaongeza tija na wilaya hiyo kushika  nafasi ya kwanza kitaifa

Akijibu ombi hilo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema atatoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya kikao na wawekeza wa madini na kutoa elimu ya tozo asilimia 2 wanayokatwa ili kuwa na mahusiano mazuri kwa kulipa kodi serikalini.

Mmoja wa wachimbaji ambaye hakutaka kuandikwa jina amesema kuwa utitiri wa tozo umepelekea baadhi yao kutorosha dhahabu ili kuweza kupata faidi kuliko kuchangia mapato.

No comments:

Post a Comment