Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa amehamasisha wananchi na vyama vya siasa kusimamisha wagombea kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Issa ambaye ni Diwani wa Kata ya Isanga mesema leo Oktoba 14, 2024 mara baada ya kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura kwenye mtaa wa Ilolo Kata ya Isanga Jijini hapa.
Amesema kuwa ni wajibu wa vyama vya siasa kuhamasisha wananchi kushiriki kuanzia zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa kuanzia hatua uandikishaji katika dafrari la wapigakura.
"Nitoe rai kwa wananchi na vyama vya siasa kushiriki kikamilifu ili kutumia fursa za kuchagua viongozi bora watakao kuwa chachu katika kuleta maendeleo" amesema.
Wakati huo huo amewataka wananchi katika kata yake kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutumia haki ya kikatiba kuchagua viongozi wanaowataka na sio kushinikizwa.
Mkazi wa Isanga Juma Saidi amesema kujiandikisha kutawapa nafasi ya kuchagua viongozi bora huku wakiendelea kuhamasisha vijana pasipo kujali itikadi za vyama.
"Kama vijana tunatumia fursa ya kupita nyumba kwa nyumba kuhamasisha vijana na kuwachukua wazee wasiojiweza kuwapeleka kwenye vituo vya kupigia kura kujiandikisha.
No comments:
Post a Comment