Monday, October 21, 2024

DKT. TULIA AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA ELIMU AFYA JIJI LA MBEYA

Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na fedha za serikali kuu ,mapato ya ndani ya Halmashauri na mfuko wa jimbo.

Katika ziara yake Dkt. Tulia ameambatana na Mkurugenzi wa Jiji John Nchimbi, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa wakiwepo madiwani na watendaji wengine wa serikali.

Dkt. Tulia ambaye  ni Rais ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ameeleza malengo ya ziara yake ni kukagua utekelezaji wa miradi ya sekta ya elimu na afya sambamba na ujenzi bweni na wanafunzi wenye mahitaji maalum ya katika Shule ya Mwenge lenye uwezo wa kuchukua watu 200.

Miradi mingine ni ujenzi wa Shule ya Msingi Mwakibete, Sekondari ya Samora Masheli na kituo cha afya Mwakibete ambacho kimepunguza hadha kwa wananchi kufuata huduma umbali mrefu.

Akizungumza na wananchi kwa nyakati Dkt. Tulia amesema serikali imejipanga kujenga miundombinu ya mabweni ya wanafunzi kwa shule za sekondari na kukarabati zilizo kongwe.

"Ndugu zangu serikali itaendelea kusogeza huduma muhimu tuna kila sababu kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha utekelezaji miradi ya elimu, afya, maji na barabara" amesema.

Amesema lengo la serikali ni kuona sekta ya elimu inafanya vyema kwa watoto kupata elimu bora ili kuwa chachu kwa Taifa la kesho na kuwataka kuwapuuza wanaosema hawaoni maendeleo.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa amesema kwa kipindi cha miaka mitatu ya Dkt. Tulia Jiji la Mbeya limepiga hatua katika nyanja mbalimbali.

"Zaidi ya Sh 780 milioni zimetumika kuboresha sekta ya elimu sambamba na ujenzi wa miundombinu ya matundu ya vyoo na kuchonga madawati 10,000 ili kuhakikisha hakuna mwanafunzi anakaa chini" amesema.

Aidha amewataka wananchi kutokubali mateso ya miaka 10 iliyopita kwa kukosa maendeleo baada ya Jimbo hilo kuongozwa na upinzani.

Mkurugenzi Jiji la Mbeya John Nchimbi alisema wataendelea kutenga mapato ya ndani kwa ajili ya kutatua changamoto ikiwepo jengo la kuhifadhi maiti kichomeo kata katika zahanati ya Mwakibete jijini hapa.


No comments:

Post a Comment