Wednesday, October 16, 2024

MILIONI 15 KUTUMIKA UJENZI SOKO LA MBOGA MBOGA KATA YA ISANGA

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeanza utekelezaji wa Ujenzi wa mradi wa soko la kisasa la  mbogamboga katika Kata ya Isanga.

Mradi huo kwa awamu ya kwanza umegharimu Tsh. 15 milioni na litakapo kamilika litakuwa fursa kwa wakulima wa mbogamboga kujikwamua kiuchumu na kuongeza wigo wa masoko ya ndani na nje.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa amesema leo Oktoba 16 mwaka huu na kwamba ujenzi wa soko hilo ni sehemu ya miradi ambayo imepokelewa katika Kata ya Isanga.

"Ujenzi wa soko la mbogamboga la Isanga utekelezaji wake umeanza na uko katika hatua nzuri sambamba na miradi mingine ya uboreshwaji wa barabara na kufunga taa" amesema Issa.

Katika hatua nyingine Issa amesema katika kutekeleza sera ya elimu wamechonga madawati zaidi ya 10,000 kwa ajili ya shule zote za msingi sambamba na mkakati wa kukarabati shule zote kongwe  zilizojengwa miaka kadhaa iliyopita.

"Jiji la Mbeya sasa linakwenda kuwa la kisasa tunakwenda kulibadilisha kutokana naa vyanzo vya mapato ya ndani yote hiyo ni kutokana na uwepo wa viongozi makini akiwepo Mbunge wa Mbeya mjini,Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson" amesema.

Mkazi wa Isanga na mkulima wa mbogamboga bonde la Ilolo Salome Aloyce amesema tangu nchi ipate Uhuru hilo ni soko la kwanza la mbogamboga kujengwa katika kata yao.

"Jitihada za Diwani tunaziona kwa kushirikiana na serikali kuharakisha kuleta maendeleo kuna barabara za rami ambazo zimefungwa taa na zimeongeza usalama wa raia na mali zao" amesema.

No comments:

Post a Comment