Thursday, July 4, 2024

ALIYECHOMA PICHA YA RAIS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MIWILI


Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Rungwe mkoa wa Mbeya imemtia hatiani ni kumhukumu kutumikia kifungo cha miaka miwili Shadrack Chaula (24) au kulipa faini ya Shilingi milioni tano.

Shadrack ametiwa hatiani kwa kosa la kusambaza taarifa za uongo kupitia mtandao wa kijamii wa Tik Tok kinyume cha  kifungu cha sheria 16 ya mtandao ya kijamii.

Hukumu hiyo imesomwa leo Julai 4, 2024 na Hakimu mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Rungwe, Shamla Shehagiro baada ya mawakili wawili wa serikali, Rosemary Mginyi na Veronica Mtafya kutoa ushahidi mahakamani hapo.

Imeelezwa mahakamani hapo mtuhumiwa alitenda kosa hilo June 22 mwaka huu katika eneo la Ntokela wilaya ya Rungwe kwa kusambaza video yenye taarifa za uongo kinyume cha kifungu cha sheria 16 ya makosa ya mitandao.


No comments:

Post a Comment