Friday, July 26, 2024

KITUO CHA MIONZI KUJENGWA JIJINI MBEYA

Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani (Ocean Road) wanatajia kujenga kituo cha mionzi na kusimika mashine za kisasa.

Mkurugenzi mtendaji wa Hosptali ya Rufaa Kanda Dkt. Godlove Mbwanji amesema mara baada ya kutembelea kitengo cha huduma za mifumo ya chakula hosptalini hapo na kuona huduma mbalimbali za kitabibu zinazotolewa.

Amesema kitendo cha Serikali kubariki ushirikiano wa Taasisi ya Saratani Ocen Road Hosptali ya Rufaa Kanda kusimika mashine za mionzi utasaidia kuwapunguzia gharama wagonjwa kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.


Dkt. Mbwanji ameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwekeza na uboreshwaji wa huduma za afya kwani itasaidia wagonjwa wa saratani mikoa ya nyanda za juu kusini kupata huduma jirani tofauti na miaka ya nyuma.

Daktari bingwa wa upasuaji Dkt. Tom Edward amesema kwa kipindi cha miezi sita watano kati ya 200 wanaofika kufanyiwa uchunguzi wa saratani ufanyiwa upasuaji.

Naye Daktari bingwa mbobezi wa mifumo ya chakula Dkt. Mary Nzota ametaja sababu ya changamoto ya saratani na vidonda vya tumbo utokana na ulaji usio na utaratibu wa vyakula na kutozingatia suala la usafi na unywaji wa maji safi na salama kwa afya

No comments:

Post a Comment