Thursday, July 11, 2024

DKT. TULIA AJITOLEA KUMSOMESHA MTOTO ALIESHINDWA KUENDELEA NA MASOMO KWA KUKOSA MAHITAJI

Kijana Richard (kushoto) akiagana na Mratibu wa Tulia Trust Addy Kalinjila Mara baada ya kumkabidhi kwa uongozi wa shule ya wavulana Uwata.

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson amejitolea kukuendeleza elimu ya kidato cha tano na sita Yatima Shadrack Mwaisela (17) aliyekwama kuendelea na masomo kwa kukosa mahitaji.

Kijana Richard aliyekuwa akiishi na bibi yake mkazi wa kijiji cha Kisondela Wilaya ya Rungwe  amekabidhiwa leo Alhamisi  kwa uongozi wa Shule ya Sekondari ya wavulana Uwata kupitia Taasisi ya Tulia Trust.

Akizungumza mara baada ya kumpokea Mwanafunzi huyo Makamu Mkuu wa Shule Wavulana  Uwata, Marco Mwakanyamale amemshukuru Dkt. Tulia kwa moyo wa kumuendeleza  kielimu kufatiatia kutoka katika mazingira magumu.

"Tumempokea kijana Richard kwenye shule yetu tuna imani atafanya vyema kwenye masomo kutokana na kutoka mazingira magumu na kuomba jamii kuiga mfano wa kusaidia vijana wenye uhitaji" amesema.

Kwa upande wake Richard amesema amepokea taarifa ya kusoma Shule ya Wavulana  Uwata na kumuhaidi kufanya vizuri kwenye masomo.

"Nashukuru sana Mbunge Dkt. Tulia kuniendeleza kielimu kwani itakuwa fursa kwangu kusoma kwa bidii na  weredi mkubwa ili kuja kuwa chachu kwa taifa la Tanzania" amesema.

Mratibu wa Tulia Trust Addy Kalinjila amemtaka kijana Richard kusoma kwa bidii ili kuja kuwa na mchango kwa watu wengine wenye uhutaji.

No comments:

Post a Comment