Friday, July 12, 2024

NDELE MWASELELA AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO MBEYA DC

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (MNEC) Ndele Mwaselela amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 bora zinazoshiriki ligi ya Mama Samia Mshikamano Cup inayoendelea katika viunga vya wilaya hiyo, vifaa hivyo ni pamoja na mipira na jezi.

Mwaselela amekabidhi vifaa hivyo vya michezo kwa timu 16 Julai 11, 2024 katika ofisi za CCM mkoa wa Mbeya.

Hata hivyo Mwaselela amesema kuwa michezo ikawe chombo cha kuzitafsiri 4R za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuelezwa kwa mambo makubwa yaliyofanywa na Rais Samia katika kipindi cha uongozi wake.


“Mashindano haya ya Mama Samia Cup yaende yakawe na ujumbe tosha juu ya kazi zilizofanywa na Rais Samia, naamini hapa mpo vijana ambao ni wachezaji wazuri mtaenda kutoa ujumbe mzuri wa kueleza kazi nzuri zilizofanywa na Mama yetu samia katika kipindi chake cha uongozi kuna mambo makubwa yamefanyika muende mkatoe ujumbe mzuri wenye kuleta matokeo mazuri” amesema MNEC Ndele Mwaselela.

Pia MNEC Mwaselela ametoa wito kwa wachezaji kwenda kutumia fursa hiyo ya kimichezo Kwa kucheza Kwa utulivu na kudumisha upendo Mshikamano katika kipindi chote cha mashindano hayo.

Akielezea zaidi Mwaselela amesema kuwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi inasema chama kitaboresha sekta ya michezo sio yanga na simba wala timu kubwa zinazofahamika sekta ya michezo ni pamoja na timu zinazotoka kwenye Kata.

“Mimi nilichofanya ni kwenda kuibua vipaji kwenye kata zetu ili kuhakikisha timu hizi zinafanya vizuri harafu tunapata timu moja nzuri ya wilaya ambayo tunaweza kuitengeneza kwa baadaye ikawe timu ambayo inawakilisha wilaya ya Mbeya DC, Mbeya DC hawana timu, Kenny Gold ni ya wilaya ya Chunya tunataka mkoa wa Mbeya uwe timu zaidi ya saba kama wanavyofanya mikoa mingine kwa hiyo tunataka kuona timu zinaanza kuibuka mapema, utaibua vipi hivyo lazima uitishe wadau wa michezo wa wilaya walete timu za kata zote 32, wakatafuta na kuwa kwenye mzunguko wa 16, bora ndo tulisema tutatoa jezi na mipira hivyo gharama zote za kuwapeleka uwanjani wachezaji zote tumetoa" amesema Mwaselela.

Hata hivyo Mwaselela amesema kuwa mshikamano ya Mama Samia yaendelee kuhubiri 4R za Mama Samia pamoja na umoja na mshikamano na kuwa Tanzania bila mshikamano hatuwezi kufanya vizuri hivyo ni venma amani iwepo.

“Tumeleta Taasisi hapa ya Mwaselela kama mdhamini Mwaselela ni yeye kama mnavyomuona ni kiongozi wa taasisi tunayo Taasisi yetu ya shule tunavyowaanzisha watoto wetu shule tunataka hata mitaani wajue kuwa Paradise Mission inapenda kuboresha michezo kwa vijana na leo mnaona vijana hapa nao watapatiwa jezi na mipira.

Kwa upande kiongozi wa Timu hizo Hamphrey Mwashibanda amesema kupitia ligi hiyo watatengeneza timu moja ya wilaya ambayo MNEC Mwaselela awapeleke wakafanye majaribio kwenye timu kubwa ili waweze kujijenga zaidi kimichezo na kupata uzoefu zaidi .

No comments:

Post a Comment