Monday, July 22, 2024

TULIA TRUST YAMSAIDIA KIJANA ALIYESHINDWA KUJIUNGA NA KIDATAO CHA TANO KWA KUKOSA MAHITAJI

Taasisi ya Tulia Trust imetoa tabasamu kwa Mussa Mwashilindi (17) akiyekwama kujiunga kidato cha tano kwa kukosa mahitaji ikiwepo sare za shule, daftari na mengineyo.

Mussa ambaye anaishi dada yake na wadogo zake wawili baada ya mama yao mzazi kufariki ghafla na kuwaacha wakijitegemea wenyewe kuendesha maisha.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi mahitaji hayo, ofisa habari kutoka Idara ya habari taasisi ya Tulia Trust Addy Kalinjila amesema mwanafunzi huyo alichaguliwa kujiunga kidato cha tano shule ya sekondari ya Dkt. Tulia iliyopo Kata ya Itende Mbeya Mjini.

Miongoni mwa mahitaji yaliyotolewa ni pamoja na fedha taslimu kwa ajili mahitaji mengine hususan sare za shule ili kuanza rasmi masomo yake.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mahitaji hayo, Mussa amemshukuru Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kwa msaada wa mahitaji ya shule.

"Nashukuru sana sina cha kumlipa zaidi ya kusoma kwa bidii ili nije kusaidia ndugu zangu kutokana na changamoto tunazopitia" amesema Mwashilindi.

Wakati huo huo Taasisi ya Tulia Trust imetoa viti mwendo kwa watoto wawili wenye ulemavu katika Kata ya Iyela na Ruanda Jijini hapa sambamba na mahitaji ya chakula kwa kikongwe Laeli Sanga (80) mkazi wa Kata ya Ilomba.

Awali kikongwe Laeli alibainika baada ya wasamalia wema kutoa taarifa kwa Spika Dkt. Tulia Ackson kuhusiana na uwepo wa familia inayoishi kazingira magumu kupitia akaunti yake ya Instagram.

No comments:

Post a Comment