Friday, July 12, 2024

TULIA TRUST YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE MASHULENI

Taasisi ya Tulia Trust imeanza zoezi la ugawaji na utoaji elimu ya matumizi yaTaulo za kike wenye mahitaji maalumu kwa shule za sekondari kata 36 za Jiji la Mbeya.

Lengo ni kuwezesha wanafunzi wa kike kutoka mazingira magumu kuweza kupata elimu bora pasipo kuwa na changamoto zinazotokana na hedhi.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, Meneja wa Taasisi ya Tulia Trust, Jackline Boaz amesema watazifikia kata tano Mbeya mjini kwa kutoa taulo za kike.

Amesema zoezi hilo litanufaisha kwa wanafunzi wa kike kutoka kaya maskini ambao wamepewa taulo za kike 550 sambamba na viatu pea 50.

"Hatutaishia leo bali ni zoezi endelevu kwa Taasisi ikiwa ni maelekezo ya Mkurugenzi wa Taasisi ambaye ni Spika wa Bunge, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson kuona mtoto wa kike anakuwa salama" amesema.

Amesema Dkt. Tulia ni mtoto wa kike ambaye amesimama kwa kuona mtoto wa kike anakuwa bora kwa kutimiza malengo yao ya kupata elimu bora na kufikia ndoto zao.

Mwanafunzi Rehema Jafet amesema wanakumbana na changamoto kubwa sana za ukosefu wa taulo za kike kujisitili pindi wakiwa hedhi kutokana na familia wanazotoka kuwa na kipato duni.

"Tunamshukuru Dkt. Tulia kwa kuona changamoto zetu tukiwa hedhi tunakosa uelewa wa masomo kwa kuwa na hofu wa kuchafuka kwa kukosa taulo za kike kitendo cha kupata hizo taulo kutarejesha uelewa" amesema.

No comments:

Post a Comment