Monday, July 1, 2024

KATA 13 JIJI LA MBEYA ZANUFAIKA NA MICHE YA PARACHICHI 1,120 BURE

Miche zaidi ya 1,120 ya matunda aina ya parachichi kwa wananchi katika kata 13 jijini Mbeya kati ya 36 zitakazo nufaika kwa lengo la uzalishaji wa kiuchumi na kutunza mazingira.

Miche hiyo imetolewa na Taasisi ya Tulia Trust kupitia Mkurugenzi wake Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni mikakati yake ya kuifanya Mbeya kuwa ya kijani.

Akikabidhi miche hiyo kwa wananchi, watendaji wa Serikali na viongozi wa chama Mratibu wa zoezi hilo na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi hiyo, Addy Kalinjila amesema hilo ni zoezi endelevu na miche hiyo inatolewa bure.

Amesema lengo la kuhamasisha Wananchi kutunzaji mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda miti yenye faida zaidi ya moja ili kujiongezea kipato kupitia zao la parachichi kutokana na mahitaji kuwa makubwa nchini na soko la uhakika.

Ametaja Kata zilizonufaika ni pamoja na Iganjo, Iduda, Igawilo, Nsalaga, Itezi, Isyesye, Ilomba, Mwakibete, Tembela, Mwasanga, Iyela, Sinde na Iganzo ikiwa ni awamu ya tatu baada ya awamu ya kwanza kutoa miche zaidi ya 1000.

Kalinjila amehamasisha viongozi hususan wataalamu wa kilimo kutoa elimu kwa wanufaika waliopata miche ya parachichi kuitunza na kuhudumia vizuri ili ije kuwa lulu katika suala la lishe kwa jamii kuondokana na utapia mlo.

Kwa upande wake mkazi wa kata ya Iganjo Joel Joseph amesema Dkt. Tulia ni Mbunge wa kipekee kujitoa kuhamasisha kilimo kwa wananchi, amepanda mbegu na historia ya kizazi cha sasa na kijacho.

No comments:

Post a Comment