Thursday, July 18, 2024

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YAWEKA ALAMA MUHIMU KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya wameendelea kuipongeza Serikali staili ya kipekee kwa kuboresha huduma za afya nchi katika kuwa hudumia wananchi, pia kuiunga mkono Serikali kufanya utalii wa ndani kwa vitendo kama alivyofanya Rais Dkt. Samia kwenye Filamu ya The Royal Tour.

Akiongea juu  kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa niaba Watumishi wa hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Salum Msambaji ameleza kuwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya imetumia njia hiyo pia kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji wa zaidi ya Bilioni 26 katika kuboresha Miundombinu, vifaa tiba, na mashine katika Hospitali Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya pamoja na huduma za kibingwa na bingwa bobezi.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya wameushukuru Uongozi wa Waziri Ummy Mwalimu (Mb) na wasaidizi wake wa Wizara ya Afya kwa ushirikiano na maelekezo mazuri wanaopatiwa ambapo yamesaidia utendaji kazi mzuri katika kuwahudumia wananchi wa Nyanda za Juu Kusini na nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC zikiwemo Zambia na Malawi.

Vilevile, Salumu ameeleza kuwa nia nyingine ya watumishi wa hospitali ya rufaa ya kanda Mbeya kupandisa bendera hiyo ya MZRH ni pamoja na kuitangaza Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Kitaifa na Kimataifa kutokana na  Mlima Kilimanjaro kuwa ni mojawapo ya alama ya Taifa, kuwa ni mlima mrefu zaidi barani.

No comments:

Post a Comment