Tuesday, July 23, 2024

DCEA AONYA MADEREVA KUJIHUSISHA USAFIRISHAJI DAWA ZA KULEVYA

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti  na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo ameonya madereva na makondakta  mabasi ya abiria  kujiepusha na tabia ya kusafirisha dawa za kulevya wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa na vyombo vya moto kutaifishwa.

Kamishna Jenerali, Aretas Lyimo amesema hayo mkoani Mbeya kwenye mkutano uluihusisha Kamati za Ulinzi na Usalama, wadau wa sekta ya afya na walaibu wa dawa za kulevya uliolenga uhamasishaji mapambano ya dawa za kulevya uliofadhiriwa na shirika la HJFMRI.

Amesema kwa sasa serikali imefanya mabadiliko ya sheria ya usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kutaifisha vyombo vya moto na madereva na makondakta stahiki.

Lyimo amesema lengo la kufanya mkutano huu Mkoa wa Mbeya ni kutoa elimu kwa vyombo vya dora, wadau mbalimbali wanao shirikiana nao kuonwb namna bora ya kudhibiti baada ya kubaini Mbeya kuwa lango ya kuvusha na kusafirisha dawa za kulevya kwenda mataifa mbalimbali kupitia Mpaka wa Tunduma na nchi jirani ya Zambia.

Amesema suala la mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni mtambuka na kuvitaka vyombo vya dora hususani Jeshi la Polisi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kushirikia kwenye maeneo ya mipakani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema watafanya oparesheni mbalimbali za ukaguzi wa mabasi kwa lengo la kukabiliana na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya na kuwataka wamiliki kutoa elimu kwa madereva.

Mkurugenzi mradi kutoka Nyanda za Juu Kusini kutika  Shirika la HJFMRI Dkt. Emmanuel Behamana amesema katika mapambano ya dawa za kulevya wanashikiana na serikali katika kuhakikisha walaibu wanaopatikana na maambukizi ya VVU wanapatiwa tiba ili kurejeshwa katika hali ya
kawaida.

No comments:

Post a Comment