Monday, July 22, 2024

TAMASHA NGOMA ZA ASILI MSIMU WA NANE KUTIMUA KIVUMBI SEPTEMBA 2024

Taasisi ya Tulia Trust imeandaa Tamasha la ngoma za asili laa makabila mbalimbali ya asili  msimu wa nane litalofanyika septemba mwaka huu.

Tamasha hill litashirikisha washiriki kutoka Tanzania bara na viziwani lengo ni  kuenzi tamaduni na kuonyesha uhalisia wa makabila

Ofisa habari na mawasiliano wa Taasisi ya Tulia Trust, Joshua Mwakanolo amesema leo Jumatatu Julai 22, 2024 na kwamba tamasha hilo litafanyika kuanzia Septemba 26 mpaka 28 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa zamani uliopo kata ya Iyela Jijini hapa.


Mwakanolo amesema mashindano ya ngoma za asili ni fursa kwa wajasiliamali wadogo ambao  wataruhusiwa kushiriki bure kwenye eneo la tukio kulingana na utaratibu utakaopangwa.

Amesema vikundi vitakavyoshiriki Tamasha hilo watajighatamia usafiri huku ushiriki wanawasiliana na maofisa utamaduni ngazi za wilaya.

Tamasha hilo maalum kama Trust traditional dancers festival, Mbeya Tulia Marathon, Tulia Trust cup, Tulia street talent competition, tuzo za umahili wa habari.

No comments:

Post a Comment