Friday, July 12, 2024

TULIA TRAST YAMPA TABASAMU MWANAFUNZI ELIMU YA SEKONDARI

Mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Itagano Jijini Mbeya  Sikujua Dickson (16) amemuomba Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kumsaidia ili atimize ndoto yake  kupata elimu kufuatia Mama yake mzazi kuficha sare za shule na kumfanyia vitendo vya ukatili.

Sikujua amesema leo Ijumaa Julai 12, 2024 Mara baada ya Taasisi ya Tulia Trust kumkabidhi mahitaji mbalimbali ikiwepo viatu, sare za shule sambamba na kumuondoa nyumbani kwa wazazi wake  kumuendeleza kielimu .

Sikujua amefikia kutoa ombi hilo baada ya kuchoshwa na tabia ya Mama yake mzazi kuficha sare za shule kwa lengo la kumkatisha masomo hali ambayo amesema apendezwi nayo.

"Licha ya kufichiwa sare za Shule lakini pia tunateseka sana na wadogo zangu wawili tunanyimwa chakula na tukiomba mahitaji tunaelezwa tunakamfufue baba yetu ambaye alifariki miaka kadhaa iliyopita" amesema.

Amesema kuwa ili aweze kutimiza ndoto zake anaomba msaada wa hali na mali kusaidiwa ili aweze kutimiza ndoto zake na kusaidia wadogo zake.

Diwani Kata ya Itagano, Yuda Sekabenga amekiri kupokea malalamiko ya kuhusiana na maisha ya familia hiyo.

Kwa upande wake Mwalimu wa  Taaluma  katika Shule ya Sekondari Itagano, Pascal Mathias amesem mbali ya mwanafunzi huyo kupitia changamoto za ukatili amekuwa akifanya vyema ambapo kwa mwaka jana kwenye mitihani ya mhula  alishika nafasi ya 9 kati ya wanafunzi 34 huku.

Meneja Taasisi ya Tulia Trust Jack line Boaz amesema wamebeba jukumu la kumsomesha, kumpangia nyumba na kumpa mahitaji yote.

"Nimeshangazwa na wazazi kata ya itagano kuzuia watoto kusoma wakati serikali imetoa elimu bure, Sisi Mama Taasisi tutamuendeleza elimu ya sekondari na kumpa mahitaji yote muhimu" amesema.

Wakati huo huo Boaz amekabidhi majitaji kama mchele, sukari, mahitaji mengine hususan vifaa vya michezo kwa shule ya sekondari Itagano.

No comments:

Post a Comment