Wednesday, July 24, 2024

MZRH KUBORESHA MIUNDOMBINU YA MAKUNDI MAALUM


Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya imesema itaendelea kuboresha miundombinu  rafiki ya huduma za  afya hususani upasuaji na macho kwa makundi maalum wakiwepo watu wenye  walemavu wa kusikia (viziwi).

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya (MZRH) Dkt. Godlove Mbwanji wakati akifunga mkutano ulioandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Mkoa wa Mbeya.

Dkt. Mbwanji amesema katika kuhakikisha huduma bora za afya zinaboreshwa  kwa makundi maalum Hosptali ya Kanda imekuwa ya kwanza kuwa na mkalimani wa lugha ya alama ili waweze kupatiwa huduma rafiki za afya.

"Hii ni sehemu ya maboresho ili kusaidia watu wenye  ulemavu wa kusikia (viziwi) wanapata huduma stahiki kama makundi mengine na ndio lengo kuu la serikali" amesema Dkt. Mbwanji.

Naye Mkalimani wa lugha za alama Hosptali ya Kanda (MZRH), Faraja Mbwilo amesema uwepo wake umerahisisha mawasiliamo baina ya wataalam wa afya na walemavu wa kusikia katika upatikanaji wa huduma za afya.

Naye Mwenyekiti wa chama cha wasiiona Mkoa wa Mbeya na Songwe,Yohana Mwonga ameomba makundi maalum kushirikishwa kwenye mikutano ya kiserikali na kijamii kuchangia maoni kwani wao wa haki kama jamii nyingine.

Tusajigwe Mwalweja Mwenyekiti wa Watu wenye ulemavu wa kusikia (viziwi) ameomba serikali katika ujenzi wa miundombinu ya barabara zikumbukwe harama za barabarani kwa kundi hilo kutokana na kugongwa na vyombo vya moto mara kwa mara

No comments:

Post a Comment