Monday, July 29, 2024

WANANCHI ISYESYE WAMSHUKURU DKT. TULIA KUGUSA WAHITAJI

Wananchi kata ya Isyesye jijini Mbeya wamesema kitendo cha Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson kusaidia wahitaji akiwepo mtoto kwenye ulemavu Jane Ambilikile (13) ni kujishusha kwa wananchi wasiojiweza.

Kauli hiyo wameitoa jana kwa nyakati tofauti mara baada ya kukabidhi nyumba mbili za wahitaji kwa familia ya Familia ya Damiani Mbwiga (50) na baiskeli mbili kwa walemavu akiwepo Mtoto Janeth Ambilikile (13) vilivyotolewa kupitia Taasisi ya Tulia Trust.

Akizungumza kwa niaba ya Wananchi Tabu Joel amesema kwa nafasi yake ya juu licha ya ubunge amekuwa ni kiongozi wa kipeke anawafuta machozi wanyonge wasio jiweza tofauti jamii inayo wazunguka.


"Yani hatukutajia kama wanufaika waliojengewa nyumba na walemavu kupata kitimwendo leo hii wangepata matumaini walikuwa wanapitia vipindi vigumu kwenye maisha ya kila siku kikubwa tunamuombea maisha marefu Dkt. Tulia" amesema.

Rais wa Umoja wa Mabunge (IPU) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tula Ackson ameitaka jamii kugusa wahitaji huku akiwatoa hofu serikali iko kwenye mchakato wa ujenzi wa miundombinu ya barabara za mitaa kwa viwango vya lami.

"Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuleta maendeleo ndio maana imeanza utekelezaji wa miradi ya kimkakati ukiwepo wa barabara njia nne, Maji kutoka chanzo cha mto Kiwira,Stendi Kuu ya Mabasi, Soko la kimataifa la Matola hususan barabara ya kilometa saba" amesema.

Pia amehamasisha jamii kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa na Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025 wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Mkoa wa Mbeya (M-NEC) Ndele Mwaselela amesema wamejipanga kuhakikisha kura za Rais Samia  Suluhu Hassan na Dkt. Tulia zinakuwa za kishindo kwa Mkoa wa Mbeya.

Mwenyekiti wa bajaji Jiji la Mbeya Lucas Mwakyusa ameomba serikali kutoa eneo kwa ajili ya kuchonga sanamu ya Dkt. Tulia kwa kutambua mchango wake kwa vijana.

No comments:

Post a Comment