Friday, July 5, 2024

DKT. TULIA AMGUSA YATIMA KUCHANGIA MAHITAJI YA SHULE

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU ) Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson ametoa zaidi ya Sh 500,000 kwa ajili ya mahitaji ya shule kwa  mtoto yatima aliyechaguliwa kujiunga kidato cha tano Shule ya Sekondari Isongole Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Fedha hizo zimekabidhiwa leo Ijumaa Julai 5, 2024 na Ofisa habari na Mawasilino wa Taasisi ya Tulia Trust Addy Kalinjila kwa mlemavu Richard Mwaisela (18) ambaye ni yatima anayelelewa na bibi yake  ambaye alikwama kuendelea na masomo kwa kukosa mahitaji.

"Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ameguswa kumsaidia Richard aweze kutimiza ndoto yake ya kupata elimu kwani bibi yake mkazi wa kijiji cha Mpuga kata ya Kisondela  alikosa uwezo wa kumsaidia baada ya kufaulu kujiunga idato cha tano Shule ya Sekondari ya Isongole na kushindwa  kuanza masomo " amesema Kalinjila.

Kalinjila amesema kuwa kama Taasisi wataendelea kuigusa jamii yenye mahitaji kwa kuchangia sekta ya elimu, afya na kuwezesha jamii isiyojiweza.

Kwa upande wake kijana Richard amemshukuru Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kwa kumuwezesha kupata mahitaji na kuhaidi kusoma kwa bidhii ili kutimiza ndoto zake za kupata elimu.

No comments:

Post a Comment