Wednesday, July 10, 2024

BILION 5.3 KUJENGA SOKO LA KISASA LA NDIZI RUNGWE

Serikali  Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya inatarajia kutumia zaidi ya Sh 5.3 bilioni kwa ajili ya  ujenzi wa soko la kisasa la mazao ikiwepo ndizi na parachichi.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa changamoto ya masoko ya uhakika hali iliyopelekea wakulima kushindwa kunufaika na uzalishaji

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Julai 10, 2024 na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Rungwe, Gabriel Mwakagenda kwa niaba ya Mbunge Athon Mwakagenda.

Amesema kuwa mradi huo wa soko la kisasa itakuwepo miundombinu mbalimbali ikiwepo migahawa,maegesho,Taasisi za kifedha za kitanzania na kigeni na huduma nyinginezo.

Mwakagenda amesema hiyo ni fursa kwa wakulima kuongeza thamani mazao ya parachichi kwa lengo la kuongeza wigo wa masoko ya ndani na nje ya nchi ikiwepo Zambia, Malawi na Congo.

"Hii ni fursa pekee mbali na kuwepo kwa mradi huo Mbunge ataanza ziara katika kata 12 zenye vijiji 43 kuelezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo uliofanywa na serikali ya awamu ya sita sambamba na kuanza kwa ligi ya Mwantona Cup.

Mwakagenda amesema kuwa pia kuna mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa jengo lenye ubaridi kwa kuhufadhia mazao jambo ambalo litasaidia wakulima kuongeza thamani mazao na kuzalisha kwa tija kubwa.

No comments:

Post a Comment