Thursday, February 29, 2024

WAKULIMA WA TUMBAKU WATAKA ZOEZI LA UGAWAJI WA PEMBEJEO LISIMAMIWE NA CHUTCU

Mkuu wa Wilaya ya Chunya ,Mbaraka Batenga akizungumza na Wakulima wa Tumbaku Wilaya ya  Chunya na Songwe katika Mkutano Mkuu wa 24 wa mwaka.

Vyama vya Ushirika vya Wakulima wa tumbaku Wilaya ya Chunya na Songwe wamekerwa na  Muungano wa Vyama Vikuu vya Ushirika Tanzania (TCJE) kuchelewesha pembejeo za kilimo na kutaka  usambazaji ufanywe na Chama Kikuu cha Wakulima wa Tumbaku (CHUTCU) ili kunusuru uzalishaji.

Kauli hiyo imetolewa jana February 29, 2024 kwenye Mkutano mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (CHUTCU) ambapo wamedai TCJE kutowafikishia mbolea kwa wakati wakuwa chanzo cha kusababisha mazao yao yasifanye vizuri shambani. 

Meneja Mkuu wa Chama cha kikuu cha wakulima wa Tumbaku (Chutcu)Wilaya ya Chunya Christian Msingwa (kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Chunya  Mbaraka Batenga.

Mkulima na Mwanachama wa CHUTCU, mawazo mamboleo amesema changamoto ya TCJE kuchelewesha pembejeo zimekuwa zilizoathiri kwenye uzalishaji wa tumbaku na hawakubaliani na TCJE kuendelea kusambaza pembejeo za kilimo badala yake chama kikuu cha ushirika CHUTCU ndio kiwe kinasimamia.

"Siku zote mnunuzi anaangalia ubora wa zao husika na madaraja sasa inapofika wakati mkulima anakwamaa katika hatua za awali za uzalishaji kuna uwezekano mkubwa wa kupata hasara,” amesema.

Kwa upande wake meneja wa TCJE, Benedict Kisaka amekiri kuchelewa kwa mbolea ya CAN na UREA, pamoja na baadhi ya pembejeo zingine zikiwepo kamba za kufungua Tumbaku nakueleza kuwa hiyo inatokana na mfumo wa uagizaji nje ya nchi ambapo amesema amewaambia wanacha wa chama kikuu cha Ushirika kuwa kamba zinatarajia kufika mwezi Machi.

Kaimu mrajisi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Mbeya aliwasisitiza wanachama kufuata taratibu na miongozo iliyowekwa na serikali katika kuendesha vyama vyao.

Sebastian Masika ni Mwenyekiti wa vyama vya ushirika Chunya (CHUTCU) aliwashukuru viongozi wa TCJE kufika kwenye mkutano huo kwani alikuwa akitupiwa lawama na wanachama kuhusiana na changamoto ya mbolea na kueleza kuwa kwa sasa wanachama wamepata majibu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Chunya Mbaraka Batengaamesema viongozi wa CHUTCU na TCJE kuhakikisha wanatatua changamoto ya upatikanaji wa pembejeo kwani changamoto hiyo imekuwa ikichonganishla wananchi na serikali.

"Hakikisheni changamoto hiyo inatatuliwa kwa wakati kwani kipimo cha uongozi wenu kitapimwa kutokana na utendaji wenu wa kazi kwani mnapoharibu kwenye vyama vyenu huko lawama zinakuja Serikalini” amesema  Batenga.

Christian Msingwa Meneja Mkuu wa CHUTCU Wilaya ya Chunya ametaja miongoni mwa changamoto zinazowakabili ni baadhi ya wakulima kutorosha Tumbaku na kwenda kuuza kwenye vyama ambavyo hawajakopa hali inayochangia kukwamisha ustawi wa uchumi wao.

“Hiyo ni changamoto kubwa inayokwanisha uchumi wao na badala yake watumie mfumo mzuri uuzaji wa zao la tumbaku na kuachana na tabia ya kutorosha ili kuweza kujiinua kiuchumi” amesema.

No comments:

Post a Comment