Monday, August 26, 2024

MEYA ISSA: DKT. TULIA MBUNGE MAKINI, MAHIRI KULETA MAENDELEO MBEYA

Mstahiki Meya Jiji la Mbeya Dourmohamed Issa, amesema umahili wa Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson ameleta mabadiliko makubwa kwa Jiji la Mbeya katika kuleta maendeleo ya miradi ya kimkakati.

Issa amesema mara baada ya kushiriki mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa 2024 wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye  mradi wa Maji Itagano - Mwanswekwa wenye thamani ya Sh 5 bilioni wenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni mbili kwa siku.

Amesema Dkt. Tulia ni Mbunge wa kitofauti kwa mahiri na umakini na amekuwa anafikika namna ya kulipambania jimbo la Mbeya kuleta maendeleo ikiwepo utekelezaji wa mradi huo wa Maji ambao utakuwa na tija kubwa kwa wananchi.

"Nina kila sababu ya kumsemea Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia kwa umahiri wake wa kuleta maendeleo ya wananchi wake kwa kuhakikisha anafanya kazi  usiku na mchana kuwaza namna gani anakwenda kuibadilisha Mbeya" amesema.

Wakati huo huo Issa amewataka wananchi kushirikiana kikamilifu kumuunga mkono sambamba na kushiriki katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa na Mkuu 2025.

Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2024, Godfrey Mnzava amesema ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Maji wa Itagano - Mwansekwa ambao unatekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mbeya-UWSA).

No comments:

Post a Comment