Sunday, August 4, 2024

TaCRI YAJA NA MIKAKATI KUKABILIANA NA KONOKONO KWENYE KAHAWA


Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Tanzania (TaCRI) imesema imekuja na mikakati ya kudhibiti wadudu waharibifu wa zao hilo wakiwepo konokono.

Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Kanda (TacRI) Dismas Pangalas kwenye viwanja vya John Mwakangale vya maonyesho sikukuu ya wakulima Nanenane ambayo  yanafanyika kikanda mkoani hapa.

Amesema wadudu aina ya konokono wamekuwa na athari kubwa na tathimini za awali zinaonyesha kuwepo kwa mashambulizi yanaweza kusababisha kupoteza miche ya kahawa huku asilimia mbili mpaka tatu uharibiwa.

Amesema hali hiyo imesababisha watafiti na wadau kutoka bodi ya Kahawa kushirikiana kutoa elimu kwenye vyama vya msingi 24, kwa mikoa ya Songwe na Mbeya katika kuelimisha wakulima mbinu za kukabiliana na konokono.

"Mbali na changamoto hizo uzalishaji umeongeza ambapo awali ilikuwa tani 25,000 na sasa imefika wastani wa tani 50,000 mpaka 80,000 na kuweka malengo kitaifa kufika tani 300,000.

Mtafiti na Mkufunzi wa TacRI Charles Mwingira amesema licha ya kufanya utafiti wameweka mikakati maalum ya usambazaji wa teknolojia ili kuleta bora kwa haraka.

Mwingira amesema hivi karibuni kuna mdudu maarufu kama 'Luhuka' amekuwa akisumbua zao la kahawa ingawa kwa mikoa ya nyanda za juu kusini ajaleta madhara makubwa huku wakiwa tayari wameanza kutoa elimu kwa wakulima kutumia pombe za kienyesha kumvuta.

Kwa upande wao wakulima walioshiriki maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane ambayo kikanda yamefanyika Mkoa wa Mbeya wamesema teknolojia ya kudhibiti wadudu waharibifu wa kahawa utasaidia wakulima kujipanga katika msimu ujao.

Annael Mwashambwa amesema TaCRI waweke mfumo wa kutoa elimu kwa wakulima vijijini ili wazalishe kwa ubora na kuchuma matunda ya kahawa yaliyo na viwango.



No comments:

Post a Comment