Friday, August 9, 2024

JIJI LAAGIZWA KUTOA HATI KWA WANANCHI WALIOKUMBWA NA MAPOROMOKO YA TOPE

Halmashauri ya Jiji la Mbeya imetakiwa kutoa hati miliki za viwanja kwa wathirika wa maporomoko ya tope la mlima Kawetere kata ya Itezi jijini hapa.

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa Agosti 9 mwaka huu mara baada ya Dkt. Tulia kufanya mkutano na waathirika hao kutatua mgogoro wa kujenga katika eneo walilopewa  viwanja kwa ajili ya makazi.

Sambamba na hilo Mbunge huyo na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) pia amekabidhi kitita cha Sh. milioni 25 zilizotolewa na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake UWT Mary Chatanda.

Amesema awali baada ya kutokea maporomoko ya tope kutoka mlima Kawetere serikali ilitoa  maelekezo ya wananchi hao kupewa viwanja na sio kulipia hati miliki.

"Wapo waathirika 16 lakini kati ya hao baadhi wamelipia hati, sasa waliolipia warejeshewe fedha zao kwani lengo na Rais Samia Suluhu Hassan wapewe viwanja bure" amesema.

Amesema mbali na hilo amesema kati ya 16 vilivyotolewa kwa wananchi na Halmashauri ya Jiji watu 11 wapimiwe viwanja vingine huku watano kati ya hao wabaki eneo walilopewa na kuwa na hati.

"Niwatoe wasiwasi wananchi serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iko pamoja nanyi na ndio maana tunawafuatilia kujua hatma yenu ikiwepo kuwa sehemu salama" amesema.

Awali mwathirika wa maporomoko, Shadrack Elias amesema kimsingi hawapo tayari kujenga katika viwanja vilivyopimwa kwani vipo ndani ya mita sitini za hifadhi ya mto.

"Huku tuliko pimiwa viwanja hakuna huduma za msingi ni kama tumetupwa polini tunaomba kupitia Mbunge wetu Dkt. Tulia haki itendeke" amesema.

Naye Diwani wa kata ya Itezi, Shambwee Shitambala ameshukuru busala za Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson kwa kutatua mgogoro huo kwani maeneo waliyopimiwa viwanja wananchi wake sio rafiki.

No comments:

Post a Comment