Friday, August 16, 2024

MKANDARASI WA MRADI MTO KIWIRA ATAKIWA KUONGEZA KASI

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amemtaka mhandisi mshauri wa Kampuni ya  GKW Consult GmbH kuharakisha ujenzi wa usanifu wa chanzo cha Maji Mto Kiwira Wilaya ya Rungwe kabla ya msimu wa kifuku kuanza.

Mhandisi Mwajuma amesema leo Mkoa wa Mbeya katika ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa chanzo cha Mto Kiwira na tenki la Maji katika eneo la New Forest.

Amesema mhandisi mshauri anapaswa kuongeza nguvu ya ujenzi ili kwenda na kasi mvua zikianza watashindwa kutekeleza na kukamilika ifikapo Aprili 2025 kama makubaliano ya mkataba ulivyosainiwa.

"Nimetoa maelekezo kwa mhandisi mshauri kuhakikisha ujenzi wa usanifu wa chanzo cha Kiwira unaharakishwa kabla ya msimu wa mvua kuanza ili kuchukua tahadhari ya mvua nyingi msimu ujao" amesema.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji Mbeya Edna Mwaigomole amesema  bado kuna changamoto ya maji hususani katika msimu huu kuelekea kiangazi.

Amesema ujio wa mradi mkubwa wa maji kutoka chanzo cha mto Kiwira utakaozalisha licha 117 milioni kwa siku utakuwa mwarobaini wa tatizo la Maji.

Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Mhandisi Barbabas Konga amesema wanaendelea kumsimamia mkandarasi na mhandisi mshauri ili kuhakikisha ifikapo Aprili 2025 mradi huo utakuwa umekamilika na kutoa huduma kwa jamii.

Amesema utekelezaji wa mradi huo kwa sasa uko asilimia 88 ambao mkataba wake unatekelezwa kwa miaka miwili tangu Aprili 2022 na ifikapo Aprili 31, 2025 utakamilika na kuanza kutoa huduma kwa watanzania.

No comments:

Post a Comment