Wednesday, August 14, 2024

"JIJI WEKENI MFUMO MZURI WA BAJAJI KUSHUSHA ABIRIA STENDI KUU" MWASELELA

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa (NEC) Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela  ameutaka uongozi wa halmashauri ya Jiji kuweka mfumo mzuri wa ulipaji wa ushuru wa madereva bajaji na kuwaruhusu kushusha abiria stend kuu ya mabasi ya mikoani.

Mwaselela amesema leo Agosti 14 mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya tatu tangu akutane na madereva wa bajaji jiji la Mbeya zaidi ya 2,000 kwa lengo la kusikiliza kero zao.

Amesema miongoni mwa kero alizopokea na kuzitolea majibu  ni pamoja na  bajaji kuzuiwa kuingia kushusha abiria ndani ya stendi kuu hali  hali ambayo inahatarisha usalama wa abiria .

"Kuna eneo ambalo wametengewa lakini wamelalamikia sio rafiki ambalo sambamba na sehemu za maegesho ambayo itakuwa na maelekezo ili waweze kulipia" amesema.


Mwaselela amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Samia Suluhu Hassan ni sikivu inayotaka kuona mtu au watu wasinyanyaswe.

"Ndio maana juzi nilikutana nao kufanya mkutano wa kusikiliza kero nimepokea na nimetoa maelekezo kwa uongozi wa wilaya na Jiji ambao tayari wameanza kufanyia kazi ikiwepo mfumo mzuri wa ulipaji ushuru wa bajaji kuingia stendi kuu ya mabasi ya mikoani" amesema.

Mwaselela pia amechangia umoja huo shilingi milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi sambamba na tofari 2,000 Ili kuwezesha kujiendesha sehemu salama.

"CCM tuko kutekeleza 4R za Rais Samia Suluhu Hasssan katika kutekeleza ilani kwa kugusa kundi la vijana kuona wanakuwa na shughuli za kufanya kwa tunaguza nyanja mbalimbali kwa kuimarisha uchumi endelevu" amesema Mwaselela.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Lucas Mwakyusa amesema kikubwa wanashukuru kwa serikali kusikia kilio chao na kuweka mwongozo.

No comments:

Post a Comment