Friday, August 9, 2024

DKT. TULIA AWATOA HOFU WAFANYABIASHARA WA SOKO LA IGAWILO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wafanyabiashara wa Soko la Igawilo lilolopo Kata ya Igawilo Jijini Mbeya kuendelea kufanya shughuli zao kwa amani ili kujipatia vipato vyao.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Agosti 8, 2024 wakati alipofanya ziara ya kuwatembelea Wafanyabiashara wa soko hilo kwa lengo la kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi ambapo miongoni mwa kero walizomtajia ni pamoja na ubovu wa miundombinu, tozo za Halmashauri pamoja na muingiliano baina ya Wafanyabiashara wa ndani na nje ya soko hilo ambapo amewahakikishia kuzitatua kwa kushirikiana na Serikali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Mhe. John Nchimbi, amesema kuwa Serikali imeanza kuzifanyia kazi changamoto za Wafanyabiashara hao na itahakikisha inazitatua kwa haraka. 

No comments:

Post a Comment